Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Viongozi wa CCM wakati wa hafla ya
Kulizindua rasmi Baraza la ushauri la Viongozi wakuu wa CCM Makao Makuu Mjini
Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kiwete akibonyeza kitufe kuashiria kulizindua Baraza la ushauri la Viongozi wakuu wa CCM Makao Makuu Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kiwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la ushauri la Viongozi wakuu wa CCM mara baada ya kulizindua rasmi Makao Makuu Mjini Dodoma.Kulia yake ni Mzee Ali Hassan mwinyi, Mzee John Malecela,Rais wa Zanzibar Dr. AIi Mohammed Sheni na Mh. Mizengo Pinda. Na Kushoto ya Dr. Kiwete ni Mh. Benjamin Mkapa, Dr. Amani Abeid Karume na Mh. Pius Msekwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kiwete akiingia katika viwanja vya Makao Makuu wa Chama hicho Mjini Dodoma akiwa ni viongozi wa Baraza la ushauri la Viongozi wakuu wa CCM alilolizindua rasmi.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mh. Benjamin William Mkapa akibadilishana mawazo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume katika hafla ya uzinduzi ya Baraza la Ushauri la Viongozi wakuu wa CCM Mjini Dodoma.
Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Makamu mwenyekiti wa CCM na Rais nwa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni katika hafla ya uzinduzi ya Baraza la Ushauri la Viongozi wakuu wa CCM Mjini Dodoma.

Press Release:-
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinzuzi
Taifa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
alisema kuundwa kwa Baraza la ushauri la Viongozi Wakuu wa Chama Cha Mapinduzi
ni fursa maalum na nzito itakayosaidia
kuimarisha zaidi nguvu ya Chama hicho.
Dr. Kikwete alisema hayo katika hafla
maalum ya uzinduzi wa Baraza hilo linalojumuisha Wenyeviti, Makamu wenyeviti na
Makatibu wakuu wastaafu wa Chama hicho iliyofanyika katika viwanja vya Makamu
Makuu ya Chama hicho yaliyopo katika Manispaa ya Dodoma.
Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa
alifahamisha kwamba Wajumbe wa Baraza hilo watakuwa na uwezo kamili wa kushauri
hata kuingia katika Vikao vya Juu vya CCM katika masuala mazito
yatakayokijengea mustakabala mzuri wa baadae chama hicho.
Dr. Kikwete alieleza kuwa Uongozi wa
CCM ulifikia uwamuzi wa kuundwa kwa Baraza hilo katika Mkutano wake Maalum wa
nane Novemba Mwaka 2012 kupitia Ibara ya 127 ya chama hicho baada ya kutambua
na kuheshimu mchango wa Viongozi hao.
Alisema Wana CCM wanastahiki kujipongeza kutokana na ushauri
huo ambao uliwahi kupingwa wakati wa nyuma kwa hofu ya Kikundi hicho
kutengeneza fitina za kumuingilia Rais katika maamuzi mazito.
Dr. Kikwete alisema Tanzania imepata
mafanikio makubwa kutokana na mabadiliko ya Kiuchumi na hata utulivu wa kisiasa
kufuatia mchango wa Viongozi wastaafu ambao kwa sasa watakuwa wakitoa mawazo
yao kwa chama kupitia Baraza hilo.
Dr. Kikwete alimtolea mfano Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mzee Ali Hassan
Mwinyi kuwa ni wa kwanza wa mabadiliko ya Uchumi na Siasa ndani ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania katika miaka ya mwishoni mwa 80 na mwanzoni mwa 90.
“ Mzee Mwinyi ametuongoza katika
mabadiliko hayo ya kiuchumi sambamba nay
ale ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa NchinibnTanzania licha ya yeye kutowahi
kuufanyika kazi Mfumo huo “. Alifafanua Dr. Kiwete.
“ Ukweli tuseme mageuzi ya kiuchumi
yaliyofanyika Tanzania chini ya uongozi wa Mzee Mwinyi wengine wakimwita Mzee
Ruksa mimi ndie niliyeanza kuyafaidi
katika kazi zangu za Urais “. Alisisitiza Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete.
Aliongeza kwamba mfumo huo wa kuundwa
kwa Baraza la Ushauri la Viongozi wa Wakuu wa Chama Cha Mapinduzi litaondoa
usumbufu wa kuwapa tabu wazee hao wa kuitwa mara kwa mara katika Vikao vya
Chama kwa lengo la kupata ufumbuzi wa mambo.
Alisema kwa mujibu wa kanuni za CCM Ibara
ya 127 Baraza hilo litakuwa na uwezo kamili wa kushauri hata ndani ya Vikao vya
juu vya Chama ama kwa kushiriki wajumbe wote wa baraza au hata uwakilishi wao.
Mapema Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Abdullrahman Kinana alisema Baraza hilo linalojumuisha Marais
wastaafu wa Serikali ya Muungano na Wenyeviti wastaafu wa CCM Taifa Marais
wastaafu wa Zanzibar kupitia na Makamu
Wenyeviti wastaafu CCM Zanzibar na Bara litafanya vikao vyake kwa mujibu wa
utaratibu watakaojipangia wenyewe.
Katibu Mkuu wa CCM Kikana alisema
wajumbe wa Baraza hilo watakuwa na fursa ya kutoa ushauri kwa Serikali
zinazoongozwa na Chama cha Mapinduzi Bara na Zanzibar.
Viongozi hao wanaounda Baraza hilo la
Ushauri la Viongozi wakuu wa CCM waliopata fursa ya kuhudhuria uzinduzi huo ni
pamoja na Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa SMT awamu ya Pili Mzee
Ali Hassan Mwinyi pamoja na aliyemfuatia Mh. Benjamin William Mkapa.
Wengine waliohudhuria ni Makamu mwenyekiti
Msaafu na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mh. Pius Msekwa.
Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dr. Salimin Amour hakuhudhuria hafla hiyo kutokana na
sababu za kiafya wakati Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Phillip Mangula yeye alikuwa
na udhuru wa msiba.
Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alibonyeza kitufe maalum kuashiria kuzindua Baraza hilo hafla iliyoambatana na ngoma za
vikundi vya utamaduni pamoja na muziki wa kizazi kipya.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
24/8/2013.
No comments:
Post a Comment