Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na
Mkurugenzi wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dar es salaam
Shumbana Taufiq kabla ya kuanza ziara yake katika Taasisi za SMZ zilizopo Mjini
Dar es salaam.
Kulia yao ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Issa Mlingoti.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika jengo la Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Mjini Dar es salaam akikaribishwa na Mkurugenzi wa Ofisi hiyo Shumbana Taifiq.
Balozi Seif akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha ZBC Dar Msangu Said Mohammed alipotembelea chumbna cha Habari cha Kitengo hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Juma Ameir akimuelezea Balozi Seif namna Wizara hiyo inavyojaribu kutatua baadhi ya changa moto wanazopambana nazo watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali waliopo Dar es salaam.
Kulia yao ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Issa Mlingoti.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika jengo la Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Mjini Dar es salaam akikaribishwa na Mkurugenzi wa Ofisi hiyo Shumbana Taifiq.
Balozi Seif akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha ZBC Dar Msangu Said Mohammed alipotembelea chumbna cha Habari cha Kitengo hicho.
Kulia yake
ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Issa
Mlingoti na Kushoto yake ni Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Hassan Mitawi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Juma Ameir akimuelezea Balozi Seif namna Wizara hiyo inavyojaribu kutatua baadhi ya changa moto wanazopambana nazo watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali waliopo Dar es salaam.
Press Release:-
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi
kuona changamoto zinazowakabili watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliopo Dar es salaam zinashughulikiwa vyema kwa
kupatiwa ufumbuzi ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya kila
siku.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofanya ziara maalum ya
kuangalia shughuli za kazi za watendaji wa Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar zilizopo Dar es salaam akianzia na Ofisi ya Uratibu wa shughuli za
Serikali.
Ofisi hiyo iliyopewa mamlaka ya kuratibu uwajibikaji wa
Taasisi zote za SMZ zilizopo Mjini Dar es salaam itakuwa chini ya Ofisi Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Sheni katika baadhi ya Taasisi za Serikali
siku moja iliyopita.
Balozi Seif alisema Serikali iliamua kwa makusudi kuanzisha Ofisi
hiyo mnamo mwaka 1986 kwa lengo la kuwa kiunganishi cha upatikanaji wa huduma
za kiuchumi kiurahisi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara sambamba na mashirika
pamoja na Taasisi za Kimataifa.
Katika mbinu za kujaribu kupunguza
matumizi ya uendeshaji wa Ofisi
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali ina nia ya kulipata jengo hilo kwa
kuwasiliana na Serikali ya Muungano hata kwa njia ya kubadilishana { Butter
system } jambo ambalo gharama zinazotumika hivi sasa zinaweza kusaidia masuala
mengine.
Akizungumzia Kitengo cha Habari
kilichojumuisha Magazeti ya Serika { Zanzibar Leo }, shirika la Utangazaji
Zanzibar { ZBC } na Habari Maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza
wana Habari hao kwa umahiri wao wa kufanya kazi licha ya kuzunguukwa na
mazingira magumu ya kikazi likiwemo tatizo la usafiri .
Aliuagiza Uongozi wa Taasisi hizo
kufanya utaratibu wa kuandika mapendekezo
ya vile vifaa muhimu zaidi vya
mwanzo na kuyawasilisha Serikalini ili kuangalia namna ya kusaidia uwezeshaji.
Balozi Seif alisema kutokana na
mabadiliko ya haraka na ya kila wakati katika sekta ya Habari, watendaji wake
wanalazimika nao muda wote waende na wakati.
“ Kwa vile Serikali Kuu tumeshaamua
Sekta zetu za Habari zijiendeshe kibiashara. Sasa Baraza letu la Wawakilishi
kuanzia mwezi Oktoba katika vikao vijavyo litalazimika kulipa matangazo ya moja
kwa moja ya vituo vya Habari vya ZBC
Redio na Tv “. Alisisitiza Balozi Seif.
Aliuagiza Uongozi wa Sekta ya Habari
kufanya utafiti utakaofahamu tatizo linalosababisha matangazo ya ZBC Redio na
Televisheni kutopatikana katika maeneo ya Tanzania Bara.
“Mimi nilikuwa msikilizaji mkubwa wa
Vipindi vya Redio hasa kile cha kutoka magazetini hakinipiti ninapokuwa Dar
pamoja na matangazo ya ZBC TV. Hata nikiwa Dodoma Matangazo ya Redio nilikuwa
nikiyapa lakini sasa yote yamekatika siju kwa nini? “ Aliuliza Balozi Seif.
Mapema Mkurugenzi wa Shughuli za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dar es salaam Shumbana Taufiq alisema Taasisi
hiyo ambayo ni kiunganishi muhimu cha mawasiliano kati ya Zanzibar na Mashirika
na Taasisi za Kimataifa imekuwa na mazingira magumu ya utekelezaji wa majukumu
yake kutokana na tatizo la kutoingiziwa fedha kwa wakati.
Mkurugenzi Shumbana alisema gharama
za kupanda kwa maisha hasa katika Jiji la Dar es salaam kumewafanya watendaji
hao kuishi katika maisha ya kubahatisha suala ambalo hupunguza ari na moyo wa
uwajibikaji.
“ Wakati mwengine sisi wasimamizi
tunakuwa katika hali ya unyonge wakati hata zile fedha za pencheni kwa
wafanyakazi wastaafu zinachelewakutufikia na matokeo yake kuleta malalamiko kwa
wazee wetu hao waliopo hapa Dar “. Alifafanua Mkurugenzi Shumbana.
Nao baadhi ya watendaji wa taasisi
hizo wakiwemo viongozi wao wa Wizara na Idara wamezitaja baadhi ya changa moto
zinazokwaza utekelezaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya
kazi, usafiri pamoja na kuomba kuongezewa posho ili kukidhi mahitaji.
Awali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alizitembelea Ofisi ya Idara ya Uratibu, Kitengo cha Utawala na Rasilmali Watu,
uratibu wa misaada na Mipango pamoja na ile ya wana Habari.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
21/8/2013.
No comments:
Post a Comment