Kushoto ya
Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk,
Kulia yake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mohammed Aboud Mohammed wakiambatana na Bamalozi wa heshima wa Uingereza,
Ujerumani an Marekani waliopo hapa Zanzibar
Kikao hicho cha dharura kilifanyika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar na kushuhudia pia na baadhi ya Viongozi wa Jumuia za utembezaji watalii za hapa Zanzibar ZATO na ZATI.
Kikao hicho cha dharura kilifanyika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar na kushuhudia pia na baadhi ya Viongozi wa Jumuia za utembezaji watalii za hapa Zanzibar ZATO na ZATI.
Press Release:-
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imesikitishwa na kitendo kibaya na kiovu walichofanyiwa raia wawili wa kike wa
Uingereza Katie Gee na Kisty Trup cha kumwagiwa Tindi kali { Acid } mapema jana usiku katika maeneo ya
Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Raia hao wawili wa Uingereza ambao
wamekuja Nchini Tanzania kwa kazi za kujitolea wakiwa hapa Zanzibar kwa
matembezi ya wiki wamejeruhiwa katika sehemu zao za uso na vifua na watu ambao
mpaka sasa bado hawajajuilikana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
wakati akizungumza na Mabalozi wadogo wa Heshima wa Uingereza, Ujerumani na
Marekani waliopo hapa Zanzibar walioambatana na Uongozi wa Wizara ya Habari,
Utamaduni Utalii na Michezo pamoja na Jumuia zinazojihusisha na utembezaji watalii
za ZATO NA ZATI.
Balozi Seif alisema kwa kuwa hilo sio
tukio la bahati mbaya kufanya hivyo amewaomba wananchi popote pale walipo
kujaribu kusaidia kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi mara tuu watakapoona
dalili za watu waliohusika na vitendo hivyo.
Alifahamisha kwamba Zanzibar ni moja
ya Nchi inayosemwa vizuri katika Nyanja za Kimataifa, lakini kwa mfumo huu
uliojichomoza unaofanywa na baadhi ya watu wachache wasioeleweka malengo yao
unaweza kukatisha tamaa kwa wale wageni waliojipangia kutaka kutemebelea
Zanzibar.
“ Ipo kumbu kumbu hapo nyuma na
nyengine si ya muda mrefu ya matukio ya baadhi ya watu kumwagiwa tindi kali {
Acid } lakini hichi cha wageni hawa waliokuwa kujitolea hapa Nchini kimewafanya
kupewa adhabu wasiyostahiki “. Alielezea Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif amewahakikishia Mabalozi hao wadogo wa Heshima hapa Zanzibar wa
Uingereza, Ujerumani na Marekani kwamba Serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya
ulinzi kwa msaada wa Wananchi itafanya uchunguzi na kuhakikisha wahusika wa
kitendo hicho wanatiwa nguvuni ili kupelekwa katika vyombo vya sheria.
Mapema Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema Vijana hao wa kujitolea kutoka
Uingereza Katie Gee na Kisty Trup walipatia huduma ya kwanza katika Hoteli ya
Tembo iliyopo Forodhani chini ya usimamizi wa Dr. Saleh Mohammed Jidawi Katibu
Mkuu Wizara ya Afya.
Alisema tukio hilo la tindikali
linaloonekana kutumiwa na baadhi ya wakorofi kama sialaha kwa kuwaathiri watu
wasio na hatia limeleta athari kubwa na kutia doa katika sekta ya Uchumi.
Waziri Mbarouk alimpongeza Balozi wa
Heshima wa Uingereza hapa Zanzibar
Balozi Carll Salisbury kwa hatua zake za kutoa usafiri wa Ndege ili
kusafirishwa kwa vijana hao ili kuendelea kupatiwa matibabu zaidi Mjini Dar es salaam na baadae
Nchini mwao.
Wakichangia katika kikao hicho Ofisa wa Ubalozi wa Marekani hapa
Zanzibar Jefferson Smith na Balozi wa
Heshima wa Uingereza hapa Zanzibar Carll Salisburg walisema Serikali ni vyema
ikawa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wakati yanapotokea matukio yasio ya
kawaida ndani ya Jamii.
Nao wawakilishi wa jumuiya za
watembezaji watalii hapa Zanzibar wameiomba Serikali kutenga fungu maalum kwa
ajili ya kuviunga mkono vyombo vya ulinzi katika kukabiliana na matukio
yanayoashiria kutaka kuvunja amani na kuhatarisha maisha ya Jamii.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed ameiasa jamii
kujenga tabia ya kuchukia jambo lolote baya lionaloonekana kujichomoza miongoni
mwao katika maeneo wanayoishi.
Waziri Aboud alieleza kwamba
mazingira yaliyopo mitaani hivi sasa yamejidhihirisha wazi kuwa wapo baadhi ya
watu wanaoshabikia matendo maovu yanayofanyika katika sehemu zao ambayo
wanaelewa wazi kuwa hatma ya matendo hayo hufikia hatua ya kuwaathiri hata wao
wenyewe.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
8/8/2013.
No comments:
Post a Comment