Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 31 wa
Kimataifa wa Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya Afrika wakifuatilia hotuba ya
ufunguzi wa Mkutano huo iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi kwenye hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano wa 31 ya Kimataifa wa Tathmini ya Elimu ya Afrika unaofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha.
Balozi Seif akiangalia maonyesho na kupata maelezo ya mfumo wa utayarishaji wa mitihani na vyeti kutoka kwa wataalamu wa Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya Afrika mara baada ya kuufungua mkutano wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya Afrika Dr. Joyce Ndalichako mara baada ya kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano wa 31 ya Kimataifa wa Tathmini ya Elimu ya Afrika unaofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha.
Balozi Seif akiangalia maonyesho na kupata maelezo ya mfumo wa utayarishaji wa mitihani na vyeti kutoka kwa wataalamu wa Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya Afrika mara baada ya kuufungua mkutano wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya Afrika Dr. Joyce Ndalichako mara baada ya kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo.
Press
Relese:-
Mataifa ya Bara la Afrika yana wajibu wa kuhakikisha kwamba
Elimu inayotolewa na kufundishwa katika Taasisi zote za Elimu Barani humu
inakuwa bora na kumnufaisha vilivyo Mtoto wa Afrika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alieleza hayo wakati akiufungua Mkutano wa 31 wa siku Tano wa Kimataifa wa
Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya Afrika { AEAA } unaofanyika katika Ukumbi wa
Victoria wa Hoteli ya Ngurdoto iliyopo Mkoani Arusha Tanzania.
Balozi Seif aliwaambia washiriki wa Mkutano huo kutoka Nchi
28 Barani Afrika sambamba na wadau wa Elimu wa Nchi washirika Duniani kwamba
Serikali za mataifa hayo wanachama ziangalie njia muwafaka katika kuona hadhi
na ubora wa elimu inaendelea kupatikana kwenye mataifa yao.
Alisema mara nyingi wananchi na hasa wazazi wa wanafunzi
wamekuwa wakilalamikia kushuka kwa kiwango cha elimu suala ambalo linafaa
kuchukuliwa hatua za ziada katika kupatikana kwa vifaa ambavyo ndivyo
vinavyochangia kupunguza ubora wa elimu.
Alisema hivi sasa kiwango cha elimu kinaonekana kuchuka
kinachochangiwa na ukosefu wa vifaa vya sayansi jambo ambalo linahitaji
mazingatio makubwa katika mabadiliko ya viwango bora vya elimu.
Balozi Seif alieleza kuwa Mkutano huo wa Tathmini ya Elimu
ya Afrika umekuja muda muwafaka kwa wanachama hao katika kubadilisha uzoefu wa
tathmini ya elimu ambapo utasaidia kujenga nguvu za pamoja katika kukabiliana
na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu Barani Afrika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba elimu
ndio uti wa mgongo wa maendeleo popote pale duniani, hivyo jitihada za ziada
zinapaswa kuchukuliwa katika kuona eneo hilo linajengewa mazingira mazuri na ya
uhakika.
“ Na matumaini makubwa kwenu washiriki wa Mkutano huu wa Tathmini
ya Elimu ya Afrika kwamba mtatumia fursa na nafasi ya mkutano huu kuondoka na
wazo litakalosaidia kuimarika kwa ubora wa elimu Barani Afrika ”. Alifafanua
Balozi Seif.
Aliwakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kuelewa kwamba Mataifa
ya Afrika yamejikubalisha kuimarisha Mpango wa Elimu kwa wote na Malengo ya Milenia
hadi ifikapo mwaka 2015 ikiwa ni hatua
inaozitaka nchi hizo kufikia.
Hata hivyo Balozi Seif alisisitiza umuhimu wa kukabiliana na
tatizo la kuvuja kwa mitihani ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likichangia kushuka
kwa kiwango cha elimu katika mataifa mengi dunia likiwemo Bara la Afrika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitolea mfano wa mpango
wa uimarishaji wa elimu unaofuatwa Zanzibar unaofuatwa kuanzia
Maandalizi,Msingi, Sekondari hadi chuo Vyuo Vikuu unaweza kusaidia katika
baadhi ya Mataifa ya Afrika endapo utafanyiwa utafiti na Jumuiya hiyo ya
Tathmini ya Elimu ya Afrika.
Mapema Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tathmini ya Elimu ya
Afrika { AEAA } Dr. Joyce Lazaro
Ndalichako alisema lengo la Mkutano huo ni kuangalia njia bora za kuimarisha
hadhi ya Elimu katika Mataifa wanachama wa { AEAA }.
Dr. Joyce alisema kwamba Jumuiya yake imekuwa ikitumia njia
kadhaa ikiwemo kuwashirikisha wataalamu sambamba na Kamati za Utafiti ili
kuhakikisha lengo hilo linafikiwa vyema.
Alisema upo utaratibu wa kubadilishana vipindi na uzoefu
katika utunzi wa mitihani kwa hatua ya kujenga nguvu za pamoja za kuimarisha
kiwango cha elimu Barani Afrika.
Akimkaribisha Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mh. Phillip Mulugo alisema wakati umefika kwa Taasisi za elimu
kuhakikisha ongezeko la Maskuli popote pale linakwenda sambamba na ubora wa
elimu.
Mh. Mulugo alifahamisha kwamba mfumo huo ukitekelezwa kwa
pamoja unaweza kusaidia kupata wataalamu wenye kiwango kinachokubalika vyema
kitaifa na Kimataifa.
Mkutano huo wa 31 wa Kimataifa wa Jumuiya ya Tathmini ya
Elimu ya Afrika uliojumuisha washiriki wa Mataifa 28 ya Bara la Afrika
umehudhuriwa pia na wadau wa Elimu kutoka mataifa zaidi ya kumi Duniani
zikiwemo Uingereza,Marekani, India, China na Ujerumani.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/8/2013.
No comments:
Post a Comment