Baadhi ya Viongozi na Wananchi wa Jimbo la Kitope wakimsikiliza Mbunge wao Balozi Seif hayupo pichani baada ya kula chakula cha pamoja mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Press Release:-
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kamwe isingependa kuona usalama na amani
ya Nchi inapotea kwa kuachwa kuchezewa na baadhi ya watu kwa maslahi yao
wakishindwa kuelewa kuwa ni hazina kubwa
kwa Taifa zima.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope alitoa kauli hiyo mara
baada ya kujumuika katika chakula cha pamoja kati yake Familia yake na baadhi
ya Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Kitope.
Hafla hiyo iliyoshirikisha pia baadhi
ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali wa Wilaya ya Kaskazini “ B “ ilifanyika
katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Jimbno la Kitope iliyopo Kinduni Wilaya ya
Kasakazini “ B “ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif alisema zipo nchi nyingi
duniani akazitolea mfano Misri na Syriya ambazo ndani ya siku kuu hii ya Iddi
el fitri iliyokuja baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa
zimezunguukwa na mitutu ya bunduki
iliyotanda kuimeza amani waliyokuwa nayo kabla.
“ Ukiipoteza amani ya nchi sharti uelewe kwamba ni tabu na kuirejesha
kwake tena inataka kazi kubwa “. Alisisitiza Balozi Seif.
Aliitahadharisha Jamii kuwa macho na
baadhi ya watu wanaojaribu kuwashawishi wananchi hasa vijana kupitia misingi ya Dini kuchochea
uvunjifu wa amani na utulivu uliopo Nchini.
Balozi Seif amewashukuru wananchi
waliojaribu kushawishiwa kujiingiza ndani ya shari katika kipindi cha mwezi
mtukufu wa Ramadhani kwa msimamo wao usiyoyumba wa kukataa shari hiyo.
Amewaomba wananchi na hasa waumini wa
Dini tofauti nchini kutokubali maeneo yao kuchezewa kwa kuoteshwa mbegu mbovu
za chuki, uhasama pamoja na shari.
Balolzi Seif aliwakumbusha Vijana
kuwa makini katika kujiepusha kutumiwa katika kufanya fujo na maovu kwani kila
siku mwanaadamu anapenda kuwa katika mambo mema ikiwemo suala la amani ambalo
ndilo la msingi mkuu kuliko yote.
Naye Mke wa Mbunge wa Kitope Mama
Asha Suleiman Iddi aliwaasa wazazi kuwa na
hadhari na watoto wao ndani kipindi hichi wakati watoto hao wanapoelekea kwenye viwanja vya
siku kuu.
Kwa upande wake Katibu Mpya wa Chama
cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini “ B” Subira Mohd Ameir alikipongeza kitendo
cha Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif cha kuwa karibu na wananchi wake
kwani huleta faraja.
Mapema Balozi Seif akitoa nasaha kwa
waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Sala ya
Ijumaa katika Msikiti wa Kitope amehimiza suala la kuendelezwa kwa ushirikiano ili kuleta upendo miongoni mwa
waumini hao.
Balozi Seif alifahamisha kwamba
ushirikiano umekuwa ukisisitizwa kila
wakati na kuelezwa ndani ya vitabu vya dini, hivyo waumini hao wanastahiki
kuuheshimu na kuufuata.
Siku Kuu ya Iddi El Fitri imekuja
kufuatia kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao ni wa Nne katika nguzo tano za Kiislamu
ikifuatiwa na Ile ya Hijja kwa muumini mwenye uwezo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
9/8/2013.
No comments:
Post a Comment