Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikabidhi Seti ya TV Flat Screen kwa Timu ya Soka ya Mwache Alale United baada ya kuibuka na ushindi wa godi 5 – 3 dhidi ya African Boys ya Upenja kwenye mchezo wa Fainal ya Kombe wa Zaweda.
Pambano hilo
lilichezwa katika uwanja wa Kitope na kushuhudiwa na Mbunge huyo Balozi Seif.
Picha
no:-984 ni:- Nahodha wa Timu ya Soka ya Mwache Alale Abdullghani Gullan
akipokea kikombe kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi mara
baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya African Boys ya Upenja.
Picha na
Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
Press Release:- {
Michezo }:-
Hatimae Timu ya Soka ya Mwacha Alale
United imeibuka na ubingwa wa mashindano ya Kombe la Zaweda ndani ya Jimbo la
Kitope baada ya kuilaza Timu ya African Coast ya Upenja kwa mabao 5 – 3
yaliyopatikana kwa njia ya Penalti katika pambano la fainali lililochezwa
kwenye uwanja wa Kitope.
Pambano hilo lililokuwa na ushindani mkali
kwa timu zote mbili lilichezwa kwa dakika 90 bila ya mshindi lilishuhudiwa na
wapenzi kadhaa wa mchezo wa soka wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kitope
Balozi Seif Ali Iddi.
Mabingwa hao wapya wa Kombe la Zaweda
Mwache Alale United walifanikiwa kupata
ushindi huo baada ya kufunga Penalti zote tano wakati wapinzani wao African
Boys ya Upenja wakapata Penalti tatu na kupoteza moja.
Mgeni rasmi wa pambano hilo Mbunge wa
Jimbo la Kitope Balozi Seif alikabidhi zawadi kwa bingwa wa mashindano hayo,
mshindi wa pili pamoja na zawadi
kwa timu zote zilizoshiriki katika
mashindano hayo ambayo ni ya pili kufanyika tokea kuanzishwa kwake mwaka
uliopita.
Balozi Seif aliwakabidhi mabingwa wa
Kombe hilo Mwacha Alale United Seti moja ya TV, King’amuzi chake, shilingi
300,000/- taslimu, seti moja ya jezi, mpira pamoja na Kikombe cha ubingwa.
Mshindi wa Pili African Boys ya
Upenja ikakabidhiwa shilingi laki
150,000/- Taslimu, seti moja ya jezi, pamoja na mpira wakati mshindi wa Tatu
Mahonda Kids wakaibuka na Seti moja ya jezi, shilingi 75,000/- taslim pamoja na
Mpira.
Mchezaji bora na mdogo kuliko wote katika
mashindano hayo alikuwa Said Khamis Kidagaa aliyepata zawadi ya shilingi
20,000/- taslimu na Mfungaji bora wa
mashindano hayo Abdull Nyafu wa African Coast ya Upenja alipata zawadi ya
shilingi 20,000/-.
Mchezaji bora wa mashindano hayo Ali
Alawi na Golkipa bora Siad Abdulla kutoka Timu ya Zaweda wamepata zawadi ya shilingi
20,000/- taslimu kila mmoja wakati zawadi ya shilingi 50,000/- Taslimu kwa timu
bora katika mashindano hayo ilichukuliwa na timu ya soka ya Zaweda.
Muamuzi bora wa mashindano hayo
aliibuka Haroun Kuchi aliyefanikiwa kupata zawadi ya shilingi 20,000/- taslim
pamoja na mpira mmoja mmoja kwa kila timu ilizoshiriki katika mashindano hayo.
Timu zilizoshiriki mashindano hayo ya
Zaweda Cup ni pamoja na Mbuyuni, Fujoni Boys, Mahonda Union, Kitope
United,Zaweda, Mgambo F.C, Kilimani City, Kibweni Youth Organization, New Star,
Mahonda Kids,washindi wa Pili African Boys ya Upenja na Mabingwa wa mashindano
hayo Mwacha Alale United.
Mapema Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope
Balozi Seif alikabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa Pete wanawake ambapo
bingwa ni watanashati wa Kitope waliopata shilingi laki 100,000/- Taslimu,
Mpira pamoja na Seti ya Jezi.
Mshindi wa pili wa mchezo huo wa
netball ni timu ya wanawake ya kiwengwa iliyozawadiwa shilingi laki 100,000/-
Taslimu, Mpira na Seti ya Jezi.
Akizunguma mara baada ya pambano hilo
la fainal na zawadi Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif aliwakumbusha
wana michezo nchini kuendelea kushikamana katika michezo ili kuleta upendo
michezoni na ndani ya Jamii.
Balozi Seif aliwatahadharisha wanamichezo
hao kuvitumia viwanja vya michezo kwa mnasaba wa kiungwana na ustaarabu na
kuacha tabia ya kuvifanya viwanja hivyo kuwa ni maeneo ya kuporomoshwa kwa
matusi.
“ Haipendezi kuona maeneo ya viwanja
vya michezo nchini yanakuwa sehemu ya kuporomoshwa matusi ambayo mara nyingi huelekezwa
kuwakashifu viongozi wanaowaongoza wanamichezo hao “. Aliasa Balozi Seif.
Aliwapongeza Wanamichezo pamoja na
uongozi wa Kamati ya mashindano hayo ya Zaweda Cup kwa juhudi zao zilizosaidia kukamilisha
mashindano hayo kwa amani na furaha.
Jumla ya shilingi Milioni 2,700,000/-
zimetumika kugharamia vifaa mbali mbali vya mashindano hayo ya Zaweda Cup
katika ununuzi wa TV, jezi mipira pamoja na kikombe.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
7/7/2013.
No comments:
Post a Comment