Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akikabidhi Seti ya TV kwa Katibu wa Maskani ya Tupendane iliyopo katika Kijiji cha Kazole Ndugu Machano Haji Machano kutekeleza ahadi alizotoa kwa wana CCM wa maskani hiyo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Wanachama wa CCM na Wananchi wameaswa kujiepusha na tabia ya baadhi ya watu
wenye tabia ya kuendeleza matusi na kejeli kwa viongozi wao ambayo
hujenga chuki na uhasama na hatimae kuashiria kuvunjika kwa amani na
utulivu hapa Nchini.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapionduzi
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akikabidhi msaada wa
seti za Televisheni, Mashine ya DVD na fedha za kuunganishia TV kwa
maskani ya CCM ya Tupendane na ile ya Mama Asha Balozi Maskani zilizomo
ndani ya Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini “ B”.
Balozi
Seif ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope aliyekuwa akitekeleza ahadi
alizozitoa kwenye maskani hizo alisema tabia hizo zinapaswa kutoungwa
mkono na Wananchi walioelekeza nguvu zao zaidi katika kujiletea
maendeleo yao.
Alifahamisha kwamba Jamii imekuwa shahidi
katika matukio kadhaa yaliyowahi kutokea ndani ya vipindi tofauti hapa
Nchini na kuleta uvunjifu wa amani ambayo yameacha makovu baada ya
kusababishwa na baadhi ya watu wanaoichezea amani kwa maslahi yao
binafsi.
“
Jamii itaendelea kukumbwa na matatizo na kukosa utulivu wa kimaisha
endapo Taifa hili halitaongozwa na Chama tawala cha Mapinduzi chenye
sera zinazotekelezeka na kukubalika na Wananchi walio wengi “.
Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
Mbunge
huyo wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliwakumbusha wana CCM na wananchi wa Jimbo hilo waelekeze nguvu zao
katika kujiletea maendeleo na Viongozi wao watakuwa tayari kuunga mkono
juhudi hizo.
Aliwashauri
wananchi hao na wana ccm kuanzisha vikundi vya ushirika vitakavyosaidia
kuongeza nguvu za pamoja katika kuelekea kwenye uzalishaji wa miradi
tofauti ya kiuchumi na kupunguza ukali wa maisha.
“
Ni vyema mkaanzisha vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali na mimi
wakati wote nitakuwa tayari kuvipa nguvu vikundi hivyo ili muweze
kutekeleza vyema malengo mliyojipangia ndani ya vikundi hivyo “ .
Alifafanua Balozi Seif.
Katika
utekelezaji wa ahadi hizo Balozi Seif pia alikabidhi mchango wa
shilingi laki tano kwa ajili ya ununuzi wa matofali na saruji ya
kuendeleza ujenzi wa Maskani ya Tupendane.
Halkadhalika
Balozi Seif akakabidhi seti za jezi na mipira kwa maskani zote mbili za
Tupendane na ile ya Mama Asha Balozi Maskani vifaa na vitu vyote hivyo
vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 2 na Laki Saba {2,700,000/- }.
Othaman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
7/7/2013.
No comments:
Post a Comment