Friday, 6 June 2014

balozi Seif Aipongeza Timu ya Ujamaa kwa Kupanda Daraja.




 Rais wa Klabu ya Ujamaa ya Rahaleo Othman Mussa akielezea mikakati ya Timu yake kushiriki mashindano ya 12 bora daraja la Pili Unguja mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.kushoto ya Othman Mussa ni mwenyekiti wa Klabu ya Ujamaa Ameir Makungu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiipongeza timu ya soka ya Ujamaa baada ya kupanda daraja ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
 Balozi Seif akiwa na Kombe la Ubingwa Daraja la Pili Wilaya ya Mjini, akifurahia baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake na Uongozi wa timu ya Ujamaa baada ya kulitowa Kombe hilo la Ubingwa lililonyakuliwa na wakongwe wa Soka Unguja Timu ya Ujamaa daraja la pili Wilaya ya Mjini.wa mwanzo kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi akiwa pia muasisi wa Timu pinzani dhidi ya Ujamaa Timu ya Muembeladu { Kubwa Lijalo } Mh. Abdulla Mwinyi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiipongeza timu ya soka ya Ujamaa baada ya kupanda daraja ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
Balozi Seif, akisalimiana na Viongozi wa Timu ya Ujama walipofika Ofisini kwake kumkabidhi Kombe la Ubingwa wa Wilaya ya Mjini kwa kuwa Mabingwa wa Ligi Hiyo kwa Mwaka 2014.

Timu Kongwe ya Mchezo wa Soka hapa Zanzibar Ujamaa Sports Club imejizatiti kurejea tena kwenye ligi kuu ya Zanzibar Daraja la Kwanza baada ya kuteremka kiwango chake na kufikia hadi Daraja la Tatu mwaka 2013.

Rais wa Klabu ya Ujamaa yenye mastakimu yake Mtaa wa Rahaleo Mkabala na Shirika la Utangazaji Zanzibar { ZBC – Redio } Othman Mussa alieleza hayo Wakati Uongozi pamoja na baadhi ya wachezaji wa Timu hiyo ulipofika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kumsalimia baada ya kutawadhwa rasmi kuwa mabingwa wa Soka Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Othman Mussa  alimueleza Balozi Seif ambae pia ni Mchezaji wa Zamani wa Klabu hiyo kwamba ipo dalili kubwa kwa timu hiyo kongwe kupanda daraja na kufikia malengo kutokana na ari na mashirikiano makubwa yaliyopo kati ya wachezaji na Viongozi wa Klabu hiyo.

Hata hivyo Rais huyo wa Klabu ya Ujamaa alieleza kwamba zipo baadhi ya changa moto zinazoikabili timu hiyo kwa hivi sasa ikiwa ni pamoja na gharama za huduma kwa vile wako katika maandalizi ya kujenga kambi kwa ajili ya kukabiliana na fainali ya mashindano ya  timu 12 Bora za soka Wilaya za Unguja.

Naye Katibu Mkuu wa Klabu ya Ujamaa Juma Khalfan alieleza kwamba Timu hiyo ilifikia hatua ya ubingwa baada kazi kubwa ya mashindano ya ligi ya soka ya Daraja la Tatu iliyozikutanisha takriban Timu 22 zilizomo ndani ya Wilaya ya Mjini.

Juma Khalfan alifahamisha kwamba klabu ya Ujamaa ambayo ina historia ndefu ya mchezo wa soka  hapa Nchini iliwahi kuchukuwa ubingwa wa Zanzibar wa mchezo huo katika miaka ya nyuma.

Akitoa shukrani zake kufuatia ubingwa huo walioupata Klabu ya Ujamaa wa Soka Wilaya ya Mjini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Uongozi na Wachezaji wa Timu hiyo bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha hadhi ya timu hiyo kisoka inarejea tena.

Balozi Seif alisema aliwasisitiza wachezaji wa timu hiyo kudumisha nidhamu wakati wanapokuwa michezoni kwa kutii uamuzi wa wachezeshaji soka ili lengo la kuimarisha uanamichezo lifanikiwe vyema.

“ Itapendeza na kufurahisha iwapo itafikia wakati timu yetu inatoa wachezaji wa Kitaifa na Kimataifa. Kwa nini wachezaji wetu wasifikie kiwango cha akina drogba, Eto, Song na wengineo wanaotoka ndani ya Bara la Afrika ? “. Aliuliza Balozi Seif.

Alisema kwa vile wachezaji wa Timu hiyo wameshaamua kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya 12 bora Daraja la Pili Kanda ya Unguja ataangalia uwezekano wa kuongeza nguvu zake ili wafikie lengo walilojiwekea.

Monday, 17 March 2014

Ripoti ya ajali ya Mv Kilimanjaro II

Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro II Khamis Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar
Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro II Khamis Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar
   
Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro II leo imekabidhi rasmi Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa  Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akikabidhi Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema kazi hiyo waliyopewa wameweza kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na walikuwa huru bila ya kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi yoyote.
Aidha alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi wa Zanzibar.
Hata hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa kuifanya kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi hiyo na majukumu mengine walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi hiyo walitakiwa kuikabidhi kesho na badala yake wameweza kuikabidhi leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro II, Khamis Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo wakati wa kumkabidhi  Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Rashid Seif Suleiman (mwenye kanzu) Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha - Nafisa M. Ali
Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro II, Khamis Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo wakati wa kumkabidhi Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Rashid Seif Suleiman (mwenye kanzu) Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha – Nafisa M. Ali
Aidha Mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi walizingatia uhalisia wa kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu.
Aidha alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia.
Hata hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Aidha aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala Serikali.
Naye Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki  itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika.
Bodi hiyo ya Wajumbe watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Baharini kifungu no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali ya Meli ya MV.
Kilimanjaro II iliyotokea miezi miwili iliyopita katika mkondo wa Nungwi ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja.

Mkutano wa Wawekezaji wa Israel na Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo
Baadhi ya washiriki wa mkutano wakimsikiliza  Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia
Baadhi ya washiriki wa mkutano wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano. Picha – OMR
About these ads

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini
Jamii Nchini imetahadharishwa kuwa makini katika kipindi hichi kilichoanza cha msimu wa mvua za masika ambacho kimezoeleka kuwa na matukio mbali mbali ya maafa yanayoleta athari kwa wananachi.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwafariji wananchi waliokumbwa na maafa kufuatia Upepo Mkali ulioambatana na mvua jana  jioni katika maeneo ya Kwaalamsha, Makadara na Mkele ndani ya Wilaya ya Mjini.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mbali ya mvua na upepo lakini kipindi hichi cha masika pia hukumbwa na miripuko ya maradhi tofauti ya kuambukiza jambo ambalo jamii inapaswa kujihadhari nayo.
Aliwahakikishia wananchi hao kwamba Serikali Kuu kupitia Idara yake ya Maafa ambayo iko chini ya Ofisi yake inaendelea kufanya tathmini na hasara iliyowakumbwa wananchi hao na baadaye iangalie namna ya kusaidia nguvu zitakazowawezesha  kurejea katika  mazingira yao ya awali.
“ Nimekuja na Timu yangu Katibu Mkuu, Mkurugenzi Maafa na timu yake kuanza tathmini na maafa haya na baadaye kuandika ripoti itakayotusaidia sisi Serikalini namna ya kuchukuwa hatua za kukabiliana na maafa hayo yaliyojitokeza “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi mbali mbali waliojitolea nguvu, maarifa na hata hifadhi  ya dharura kwa wenzao  waliopatwa na maafa hayo kufuatia upepo huo wa ghafla.
Alisema kitendo hicho mbali ya kuleta faraja kwa waathirika hao pamoja na Serikali kwa jumla lakini pia kimeongeza upendo na kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Wananchi hao.
“ Ukweli nimefarajika sana kusikia kwamba majirani zenu walikuwa pamoja na nyinyi muda wote wa tukio hili. Huu hasa ndio ujirani mwema unaotakiwa kuwemo ndani ya nyoyo za wanaadamu wakati wote “. Alifafanua Balozi Seif.
Wakitoa shukrani zao kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baadhi ya wananchi hao walioathirika na upepo huo walielezea kufarajika kwao na hatua zilizochukuliwa na majirani zao katika kuwasaidia kukabiliana na maafa hayo.
Nyumba zipatazo Tatu katika Shehia ya Kwaalamsha, Tano Sheria ya Mkele na nyengine kadhaa ambazo bado idadi yake hajijajuilikana katika Shehia ya Makadara zimeathirika kutokana na upepo huo.
Othman Khamis Ame – Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar akiangalia jengo la Duka la Mfanyabiashara Khadija Ame Abdulla katika Mtaa wa Kwaalamsha ambalo limeangukiwa na nguzo ya umeme kufuatia upepo mkali uliovuma katika eneo hilo
Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar akiangalia jengo la Duka la Mfanyabiashara Khadija Ame Abdulla katika Mtaa wa Kwaalamsha ambalo limeangukiwa na nguzo ya umeme kufuatia upepo mkali uliovuma katika eneo hilo
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma  na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma  na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Moja ya kati ya Nyumba  tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar
Moja ya kati ya Nyumba tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma  na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma  na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar

Sunday, 6 October 2013

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza umuhimu wa Jimbo la Kiembe samaki kurejea katika Hisotia yake ya kuwa na wanamichezo mahiri wa soka

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza umuhimu wa Jimbo la Kiembe samaki kurejea katika Hisotia yake ya kuwa na wanamichezo mahiri wa soka wakati akikabidhi Jezi na Mipira kwa timu zilizoshiriki kombe la Dr. Sheni ndani ya Jimbo hilo hivi karibuni.
Balozi Seif akimkabidhi Jezi  na Mipira Katibu wa CCM Jimbo la Kiemba Samaki Suleiman Haroub kwa ajili ya Timu 8 zilizoshiriki Dr. Sheni Cup Jimboni humo hivi karibuni ili kutekeleza ahadi aliwapa wanamichezo hao wakati akiyafunga mashindano hayo.


Uongozi wa Chama cha Mapinduzi kupitia Umoja wa Vijana wa Chama hicho wa Jimbo la Kiembe Samaki umepongezwa kwa utaratibu wake uliojipangia wa kuendesha na kuimarisha michezo hasa ule wa kandanda ndani ya Jimbo hilo.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hapo nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akikabidhi Jezi na mipira kwa  timu za  soka nane zilizoshiriki Mashindano ya Kombe la Dr. Sheni    ambayo yalifanyika hivi karibuni katika Jimbo la Kiembe Samaki.
Balozi Seif ambae alikuwa akitekeleza ahadi aliyoitowa  wakati akiyafunga mashindano hayo kwa kuipatia seti moja ya jezi na Mipira Miwili kila timu shiriki  kati ya nane  zilizomenyana kwenye  mashindano hayo alisema Kiembe samaki inapaswa kurejea katika historia yake ya kutoa wachezaji wazuri.
Alisema eneo la Kiembe samaki limekuwa likitajikana kwa kuwa na wanasoka mahiri ambao wengi kati yao walifanikiwa kuchezea timu kubwa mashuhuri hapa Nchini ikiwemo ile ya Taifa ya Zanzibar  na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wanamichezo hao wa Jimbo la Kiembe samaki kwamba  Serikali itajitahidi kuona kero zinazowakabili wana michezo hao hasa lile tatizo la uwanja wao linatafutiwa ufumbuzi.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Waride Bakari Jabu, Katibu wa CCM Jimbo hilo Suleiman Haroub alimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa umahiri wake anaoendelea kuwa nao wa kuimarisha michezo hapa Nchini.
Naye Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Kiembe Samaki Ibrahim Mbarak Ramadhan alimueleza Balozi Seif kwamba licha ya jitihada zinazochukuliwa na uongozi wa Jimbo hilo wa kuimarisha michezo lakini bado suala la ubovu wa viwanja vya michezo limekuwa kero kubwa.
Ibrahim Mbarak alifahamisha kwamba ubovu wa uwanja wao ambao pia hutumika katika  sherehe za siku kuu za Iddi umekuwa ukiwanyima furaha ya kuendeleza kwa michezo yao katika kiwango kinachokubalika Kimichezo.
“ Tunatamani uwanja wetu wenye urefu unaokubalika kivipimo siku moja unahimili tumutiwa kwa mazoezi au mashindano nyakati za usiku kama vilivyo viwanja vyengine vya wenzetu  ambavyo viko nje ya Mji Mkuu “. Alitoa joto lake katibu huyo wa uvccm Jimbo la Kiembe samaki.




Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn Klirpsvik Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
























Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn Klirpsvik  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar ambapo walipata wasaa wa kubadilishana mawazo juu ya uhusiano wa mataifa yao mawili.

Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa kujifunza kupitia Mataifa, Taasisi na Mshirika ya Kimataifa katika mpango wake iliyolenga wa kuelekea kwenye mradi mpya wa uzalishaji wa Mafuta.
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn Klirpsvik alitoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Ingunn alisema hatua hiyo ya tahadhari inayofaa kuchukuliwa na Zanzibar inaweza kuwa mwanzo mzuri wa kuingia katika mradi huo mpya wa Kiuchumi  kwenye muelekeo wa mafanikio makubwa.
Balozi huyo wa Norway Nchini Tanzania alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Norway wakati wote iko tayari kutumia ujuzi  wake mkubwa katika masuala ya Mafuta kuisaidia Zanzibar kitaalamu ili ifanikiwe katika malengo iliyojipangia katika kuendesha mradi huo.
Alifahamisha kwamba Nch hiyo imekuwa mshirika mkubwa wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla katika kuunga mkono harakati za kiuchumi na ustawi wa Jamii wa wananchi walio wengi Nchini.
“ Tumekuwa na ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu katik a pande zetu hizi mbili unaolenga kustawisha harakati za kijamii na uchumi kwa wananchi walio wengi “. Alisisitiza Balozi huyo wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn  Klirpsvik.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Norway kwa juhudi zake za kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika maendeleo hasa uungaji mkono katika miradi ya miundo mbinu ya Kiuchumi.
Akizungumzia suala la amani ambalo linaonekana kuiteteresha pembe ya Bara la Afrika Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Tanzania imelazimika kuchukuwa tahadhari ili kudhibiti wimbi hili linaloonekana kulikumba eneo hilo.
Balozi Seif alisema Serikali aya Tanzania  iko makini katika kufuatilia wageni wasio na mfumo sahihi wa kuishi ndani ya ardhi ya Tanzania na jitihada zinachukuliwa katika kuratibu wageni walioamua kuishi Nchini kupitia Sheria na taratibu zilizopo za Kitaifa na Kimataifa.
“ Tanzania imelazimika kuwa na tahadhari katika masuala  ya ulinzi wa amani ili kujaribu kuzuia au kudhibiti uasi ama ubabe unaoweza kufanywa na watu au vikundi vinavyopenda kuichezea amani “. Alisisitiza Balozi Seif.
Kuhusu suala la mchakato wa kuelea kwenye Katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi huyo wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn kwamba mabaraza ya Katiba ya Wilaya  yamekamilisha vyema mijadala yao.
Balozi Seif alisema hatua hiyo ndio iliyopelekea Bunge la Jamuhuri ya Muungano kujadili Marekebisho ya  sheria ya Katiba na kuipitisha ili kuundwa kwa Bunge la Katiba litakalojadili na  kuidhinsha i   kupigwa kwa kura ya maoni hapo baadaye ili kuamilisha mchakato mzima wa kupata katiba mpya.
Balozi Seif aliendelea kusisitiza kwamba Zanzibar imeshirikishwa kikamilifu katika mchakato mzima wa kujadili katiba hiyo kuanzia msingi licha ya malalamiko na shutuma zinazoendelea kutolewa na upande wa upinzani kwamba Zanzibar haikushirikishwa.

Wednesday, 2 October 2013

Jamii Nchini inapaswa kuendelea kusaidia Jumuiya zinazojitolea katika mapambano dhidi ya maambukizo ya virusi vya Ukimwi ili kuwapa faraja na matumaini zaidi watu ambao tayari wameshaathirika na maradhi hayo.

























Mkurugenzi wa Kampuni ya Malik Food inayojihusisha na Biashara ya Kuku { Maarufu Paja nono } Fikirini Hango akimkabidhi Mwenyekiti wa Zapha + Bibi Consolata John Boksi mbili za Mapaja ya Kuku kwa ajili ya kitoweyo cha watoto wanaoishi na vurusi vya Ukimwi.
Nyuma ya Mkurugenzi Fikirini ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Bibi Hasina Hamad pamoja na Mkurugenzi wa Zapha +.


Naibu Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Suleiman Haji Suleiman kwa Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zapha + Bibi Hasina Hamad msaada wa vyakula.
Pembeni ya Bibi Hasina Hamad ni Mkuu wa Huduma Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Kombo  Haji Kheir.
Msaada huo uliokabidhiwa hapo katika Kituo cha Jamii na Watoto cha Zapha + kiliopo Welezo umelenga kuwasaidia watoto yatima walioathirika na virusi vya ukimwi  ambao wazazi waowameshafariki Dunia.


  Press Release:-
Jamii Nchini inapaswa  kuendelea  kusaidia Jumuiya zinazojitolea katika mapambano  dhidi ya maambukizo ya virusi vya Ukimwi ili kuwapa faraja na matumaini zaidi  watu ambao tayari wameshaathirika na maradhi hayo.
Makamu  wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akikabidhi msaada wa vyakula  kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye mazingira magumu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao  wazazi wao tayari wameshafariki Dunia.
Balozi Seif alitoa msaada huo wa  Mchele, Mafuta na Sabuni uliowasilishwa na Naibu Katibu wake Nd. Suleiman Haji Suleiman  kwa Uongozi wa Kituo cha Jamii na Watoto cha Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar               { ZAPHA+ }  kiliopo Welezo.
Alisema msaada huo unatokana na ahadi aliyoitoa hivi karibuni ya kukubali kusaidia watoto wenye  mazingira magumu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao wazazi wao wameshafariki  Dunia kutokana na maradhi hayo.
Halkadhalika alieleza kwamba amepata msukumo wa kutoa msaada huo hasa ikizingatiwa kwamba siku kuu ya Iddi el Hajj inakaribia ili wapate kusherehekea vyema Siku Kuu hiyo kubwa ambayo waumini wa Dini ya Kiislamu hukusanyika Makka Nchini Saudi Arabia Kutekeleza Nguzo ya Tano ya Kiislamu kwa wale muumini mwenye uwezo.
Akipokea msaada huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zapha+ Bibi Hasina Hamad amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa uungwana wake wa kutekeleza ahadi aliyowapa ndani ya kipindi kifupi kilichopita.
Bibi Hasina alisema msaada huo licha ya kwamba hautokidhi mahitaji ya watoto hao moja kwa moja lakini inafurahisha kuona utapunguza mzigo mkubwa uliokuwa ukiukabili Uongozi wa Jumuiya hiyo katika kuwahudumia watoto hao.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wadhamini wa Zapha+ amewaomba wananchi, wahisani na wafadhili tofauti ndani na nje ya Nchi kuendelea kuunga Mkono juhudi za Jumuiya  hiyo ili ifikie lengo la kuanzishwa kwake.
“ Tunaamini kwamba wapo watu, washirika, wahisani na hata taasisi tofauti ziwe za Kijamii na hata za ziserikali ambazo zitajitokeza kuwasaidia watoto wetu hawa tukitambua kwamba hili ni jukumu letu zote jamii “. Alifafanua Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wadhamini ya Zapha+ Bibib Hasina Hamad.
Wakati huo huo Kampuni ya Malik Food inayojihusisha na biashara ya Kuku             { maarufu  Paja nono }  imeitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Zapha+  wa kusaidia watoto wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ambao wazazi wao wameshafariki Dunia.
Akikabidhi Boksi Mbili za Mapaja ya Kuku zenye uzito wa Kilo  20 zikiwa na thamani ya shilingi 80,000/- Mkurugenzi wa Kampuni ya Malik Food Bwana Fikirini Hango alisema uongozi wa kampuni hiyo umeamua kutoa msaada huo ili kuitikia wito wa Serikali wa kusaidia Jamii zenye kuishi katika mazingira Magumu.
Mkurugenzi Fikirini alisema licha ya Kampuni hiyo ya kuendesha biashara hiyo ya Kuku walio katika kiwango kinachokubalika lakini pia hujipangia utaratibu wa kutoa misaada kwa wananchi kulingana na mazingira ya mahitaji ya Jamii.
Akipokea msaada huo Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar Zapha + Bibi Consolata John aliipongheza Kampuni ya Malik Food kwa jitihada zake za kusaidia jamii hasa watoto mayatima muda wowote ule wanapoombwa kufanya hivyo.
Bibi Consolata aliikumbusha Jamii hapa Nchini kuendelea kuelewa kwamba jukumu la ulezi wa watoto wenye mazingira magumu ambao wameathirika na virusi vya ukimwi si la Jumuiya ya Zapha + pekee bali ni la Jamii yote kwa ujumla.