
Rais
wa Klabu ya Ujamaa ya Rahaleo Othman Mussa akielezea mikakati ya Timu
yake kushiriki mashindano ya 12 bora daraja la Pili Unguja mbele ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.kushoto ya Othman Mussa ni mwenyekiti wa Klabu ya Ujamaa Ameir Makungu.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiipongeza timu ya soka ya
Ujamaa baada ya kupanda daraja ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
Balozi
Seif akiwa na Kombe la Ubingwa Daraja la Pili Wilaya ya Mjini,
akifurahia baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake na Uongozi wa timu ya
Ujamaa baada ya kulitowa Kombe hilo la Ubingwa lililonyakuliwa na
wakongwe wa Soka Unguja Timu ya Ujamaa daraja la pili Wilaya ya Mjini.wa
mwanzo kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar {
BTMZ } Sharifa Khamis na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi akiwa pia muasisi
wa Timu pinzani dhidi ya Ujamaa Timu ya Muembeladu { Kubwa Lijalo } Mh.
Abdulla Mwinyi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiipongeza timu ya soka ya
Ujamaa baada ya kupanda daraja ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
Balozi Seif, akisalimiana na Viongozi wa Timu ya Ujama walipofika
Ofisini kwake kumkabidhi Kombe la Ubingwa wa Wilaya ya Mjini kwa kuwa
Mabingwa wa Ligi Hiyo kwa Mwaka 2014.
Timu
Kongwe ya Mchezo wa Soka hapa Zanzibar Ujamaa Sports Club imejizatiti
kurejea tena kwenye ligi kuu ya Zanzibar Daraja la Kwanza baada ya
kuteremka kiwango chake na kufikia hadi Daraja la Tatu mwaka 2013.
Rais
wa Klabu ya Ujamaa yenye mastakimu yake Mtaa wa Rahaleo Mkabala na
Shirika la Utangazaji Zanzibar { ZBC – Redio } Othman Mussa alieleza
hayo Wakati Uongozi pamoja na baadhi ya wachezaji wa Timu hiyo ulipofika
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
kumsalimia baada ya kutawadhwa rasmi kuwa mabingwa wa Soka Daraja la
Pili Wilaya ya Mjini.
Othman
Mussa alimueleza Balozi Seif ambae pia ni Mchezaji wa Zamani wa Klabu
hiyo kwamba ipo dalili kubwa kwa timu hiyo kongwe kupanda daraja na
kufikia malengo kutokana na ari na mashirikiano makubwa yaliyopo kati ya
wachezaji na Viongozi wa Klabu hiyo.
Hata
hivyo Rais huyo wa Klabu ya Ujamaa alieleza kwamba zipo baadhi ya changa
moto zinazoikabili timu hiyo kwa hivi sasa ikiwa ni pamoja na gharama
za huduma kwa vile wako katika maandalizi ya kujenga kambi kwa ajili ya
kukabiliana na fainali ya mashindano ya timu 12 Bora za soka Wilaya za
Unguja.
Naye
Katibu Mkuu wa Klabu ya Ujamaa Juma Khalfan alieleza kwamba Timu hiyo
ilifikia hatua ya ubingwa baada kazi kubwa ya mashindano ya ligi ya soka
ya Daraja la Tatu iliyozikutanisha takriban Timu 22 zilizomo ndani ya
Wilaya ya Mjini.
Juma
Khalfan alifahamisha kwamba klabu ya Ujamaa ambayo ina historia ndefu ya
mchezo wa soka hapa Nchini iliwahi kuchukuwa ubingwa wa Zanzibar wa
mchezo huo katika miaka ya nyuma.
Akitoa
shukrani zake kufuatia ubingwa huo walioupata Klabu ya Ujamaa wa Soka
Wilaya ya Mjini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Uongozi na Wachezaji wa Timu hiyo bado wana kazi kubwa ya
kuhakikisha hadhi ya timu hiyo kisoka inarejea tena.
Balozi
Seif alisema aliwasisitiza wachezaji wa timu hiyo kudumisha nidhamu
wakati wanapokuwa michezoni kwa kutii uamuzi wa wachezeshaji soka ili
lengo la kuimarisha uanamichezo lifanikiwe vyema.
“
Itapendeza na kufurahisha iwapo itafikia wakati timu yetu inatoa
wachezaji wa Kitaifa na Kimataifa. Kwa nini wachezaji wetu wasifikie
kiwango cha akina drogba, Eto, Song na wengineo wanaotoka ndani ya Bara
la Afrika ? “. Aliuliza Balozi Seif.
Alisema
kwa vile wachezaji wa Timu hiyo wameshaamua kuweka kambi kwa ajili ya
kujiandaa na mashindano ya 12 bora Daraja la Pili Kanda ya Unguja
ataangalia uwezekano wa kuongeza nguvu zake ili wafikie lengo
walilojiwekea.
No comments:
Post a Comment