Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya
Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za
Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini
Jamii Nchini imetahadharishwa kuwa makini
katika kipindi hichi kilichoanza cha msimu wa mvua za masika ambacho
kimezoeleka kuwa na matukio mbali mbali ya maafa yanayoleta athari kwa
wananachi.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati
akiwafariji wananchi waliokumbwa na maafa kufuatia Upepo Mkali
ulioambatana na mvua jana jioni katika maeneo ya Kwaalamsha, Makadara
na Mkele ndani ya Wilaya ya Mjini.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mbali ya mvua na upepo lakini kipindi
hichi cha masika pia hukumbwa na miripuko ya maradhi tofauti ya
kuambukiza jambo ambalo jamii inapaswa kujihadhari nayo.
Aliwahakikishia wananchi hao kwamba
Serikali Kuu kupitia Idara yake ya Maafa ambayo iko chini ya Ofisi yake
inaendelea kufanya tathmini na hasara iliyowakumbwa wananchi hao na
baadaye iangalie namna ya kusaidia nguvu zitakazowawezesha kurejea
katika mazingira yao ya awali.
“ Nimekuja na Timu yangu Katibu Mkuu,
Mkurugenzi Maafa na timu yake kuanza tathmini na maafa haya na baadaye
kuandika ripoti itakayotusaidia sisi Serikalini namna ya kuchukuwa hatua
za kukabiliana na maafa hayo yaliyojitokeza “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliwapongeza Wananchi mbali mbali waliojitolea nguvu, maarifa na hata
hifadhi ya dharura kwa wenzao waliopatwa na maafa hayo kufuatia upepo
huo wa ghafla.
Alisema kitendo hicho mbali ya kuleta
faraja kwa waathirika hao pamoja na Serikali kwa jumla lakini pia
kimeongeza upendo na kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa
Wananchi hao.
“ Ukweli nimefarajika sana kusikia
kwamba majirani zenu walikuwa pamoja na nyinyi muda wote wa tukio hili.
Huu hasa ndio ujirani mwema unaotakiwa kuwemo ndani ya nyoyo za
wanaadamu wakati wote “. Alifafanua Balozi Seif.
Wakitoa shukrani zao kwa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baadhi ya wananchi hao
walioathirika na upepo huo walielezea kufarajika kwao na hatua
zilizochukuliwa na majirani zao katika kuwasaidia kukabiliana na maafa
hayo.
Nyumba zipatazo Tatu katika Shehia ya
Kwaalamsha, Tano Sheria ya Mkele na nyengine kadhaa ambazo bado idadi
yake hajijajuilikana katika Shehia ya Makadara zimeathirika kutokana na
upepo huo.
Othman Khamis Ame – Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Balozi
Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar
akiangalia jengo la Duka la Mfanyabiashara Khadija Ame Abdulla katika
Mtaa wa Kwaalamsha ambalo limeangukiwa na nguzo ya umeme kufuatia upepo
mkali uliovuma katika eneo hilo
Baadhi
ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na
kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Baadhi
ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na
kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar
Moja
ya kati ya Nyumba tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na
kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar
No comments:
Post a Comment