SHEREHE ZA KUKABIDHI MCHANGO WA VIKUNDI VYA USHIRIKA WA WAWANAWAKE
WANAUSHIRI wa Vikundi vya Ushirika vya Wanawake Wilaya ya Chake Chake Pemba wakimsikiliza Mkle wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwahutubia katika sherehe za kukabidhi mchango uliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mama Asha Balozi na Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho Chakechake
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwahutubia Wanaushirika wa Vikundi vya Wanawake Wilaya ya Chakechake, baada ya kukabidhi misaada iliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mama Asha Balozi na Wake wa Wawakilishi na Wabunge kwa ajili ya kuegeze mtaji wa Ushirika wao.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, kushoto akimkabidhi fedha kiongozi wa Kikundi cha Ushirika cha Wanawake wa Tujiendeleze kwa Maisha Bora Hadia Omar, shiliki laki nne kwa kikundi chao.
WANACHAMA vikundi vya Ushirika vya Wanawake wakishangilia kwa kubeba zawadi zao kumpelekea Mama Asha Balozi .
Picha na Habari kutoka
Hassan Issa na Othman Khamis
Vuga newsroom
OMPR - ZANZIBAR
OMPR - ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment