Mhandisi wa Vituo vya Umeme katika shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Mohd Juma Othman akimfafanulia Balozi Seif mfumo wa ugawaji wa laini za umeme mkubwa kwenda katika vituo vipya vilivyojengwa kwa lengo la kutoa huduma za uhakika za Umeme maeneo tofauti Nchini.
Mhandisi wa Vituo vya Umeme katika shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Mohd Juma Othman akimfafanulia Balozi Seif mfumo wa ugawaji wa laini za umeme mkubwa kwenda katika vituo vipya vilivyojengwa kwa lengo la kutoa huduma za uhakika za Umeme maeneo tofauti Nchini.
Mhandisi wa Vituo vya Umeme katika shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Mohd Juma Othman akimfafanulia Balozi Seif mfumo wa ugawaji wa laini za umeme mkubwa kwenda katika vituo vipya vilivyojengwa kwa lengo la kutoa huduma za uhakika za Umeme maeneo tofauti Nchini.
Press Release
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji Nishati na Madini
imeombwa kufikiria njia muwafaka ya kuyauza Majanareta yaliyopo katika kituo
kikuu cha kupokelea Umeme Mtoni ili kuwepusha hasara endapo yataendelea kuwepo
eneo hilo bila ya matumizi.
Majanareta
hayo 30 yalikuwa yakitoa huduma za umeme wa dharura katika kipindi ambacho
Zanzibar ilikuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa huduma ya nishati ya umeme
kutokana na kinanzio chake ilichokuwa ikikitumia wakati huo kutokidhi mahitaji
halisi ya huduma hiyo Nchini.
Mhandisi wa
Maganareta katika Kituo Kikuu cha Umeme Mtoni Yussuf Reja alitoa ushauri huo
wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
kuangalia maendeleo ya uzalishaji wa huduma ya umeme Nchini kupitia miundo
mbinu iliyopo katika kituo hicho.
Mhandisi
Yussuf Reja alimueleza Balozi Seif kwamba Majanareta hayo yako katika
kiwango bora lakini tatizo kubwa liliopo
ni huduma ya mafuta ambayo ni maalum { IDO } na yana hitaji
gharama kubwa za uendeshaji.
Alisema
Shirika la Umeme lilikuwa likipata hasara ya zaidi ya shilingi Milioni
16,000,000/- kwa saa wakati maganareta
hayo yalipokuwa yakiwashwa kusaidia huduma za umeme katika kipindi cha mgao wa
huduma hiyo muhimu.
Mhandisi
Yussuf Reja alifahamisha kwamba shirika la umeme lilikuwa likizalisha umeme kupitia
Maganareta hayo kwa uniti moja yenye thamani ya shilingi 500/- ambayo ingelazimika kuwauzia wateja wake
uniti moja kwa shilingi 700/- gharama ambayo ni mzigo kwa mwananchi wa kawaida.
“ Ukweli
uliowazi gharama ya kuyaendesha Maganareta hayo kupitia shirika la Umeme ni
kubwa mno na inaweza kuleta maafa kwa shirika hilo endapo yataendelea kutumiwa
“. Alitahadharisha Mhandisi Yussuf Reja.
Naye Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji, Nishati na Madini Nd.Mustafa Aboud
Jumbe alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wizara hiyo tayari
imeshapokea mapendekezo ya Shirika hilo kuhusiana na majanareta hayo ya Kituo
cha Umeme Mtoni.
Naibu Katibu
Mkuu huyo wa Ardhi Mustafa Jumbe alisema
Wizara hiyo inajipanga kuyafanyia kazi mapendekezo hayo na baadaye kuyawasilisha
Serikali kuu kwa ajili ya kupatia ufumbuzi muwafaka.
Mapema Kaimu
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Thabit Salum Khamis alisema
mfumo mpya wa kisasa wa huduma za umeme kwenye kituo kikuu cha Umeme Mtoni
uitwao { SCADA } umewawezesha watendaji wa shirika hilo kufanya kazi zao kwa
ufanisi mkubwa.
Thabit Salum
alimfahamisha Balozi Seif kwamba mfumo huo umepunguza kero kubwa ya kukatika
katika kwa umeme kulikokuwa kukitoa usumbufu kwa wananchi walio wengi kwenye
maeneo mbali mbali wakati inapotokea hitilafu.
Alieleza
kwamba shirika la umeme limekuwa na vituo vikubwa vinavyosambaza umeme kutoka
kituo kikuu cha Mtoni kwenda Welezo na Fumba ambavyo vimepangwa kusambaza
huduma hiyo na kuacha mfumo wa zamani wa kutumia laini moja tuu.
Kaimu Meneja
huyo wa Shirika la Umeme aliongeza kwamba matumizi zaidi ya umeme huongezeka kutoka Mega walts 33.16
nyakati za asubuhi hadi kufikia Mega
Walts 48.1 kipindi cha jioni lakini
huduma hiyo kuongezeka zaidi katika kipindi cha siku kuu na kufikia hadi Mega
Walts 52.
Uwezo wa
laini mpya ya umeme uliopo Zanzibar hivi sasa imefikia Mega Walts mia moja ambapo shirika limekuwa na hakiba ya umeme
kwa zaidi ya asilimia 50% mbali ya ile laini ya zamani yenye uwezo wa mega
walts 40 kutokana na kuchakaa kwake.
Akitoa
nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwatanabahisha
watendaji wa shirika la umeme kwamba huduma ya umeme hivi sasa imekuwa nyenzo muhimu ya kiuchumi kwa vile inasaidia kipato
cha mwananchi.
Balozi Seif
alisema ni vyema kwa watendaji wa shirika la umeme kufanya kazi zao katika
mazingira ya ushindani mfano wa kuwepo mashirika mengine yanayotoa huduma hizo hapa
nchini kwa lengo la kupata ufanisi sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja
wake.
“ Watendaji
lazima mfanye kazi kama mko katika ushindani wa kibiashara na mashirika mengine licha ya kwamba mpo peke
yenu. Kila mkiamka lazima mfikirie mtaongeza vipi wateja wengine wapya “.
Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwakumbusha wafanyakazi wa shirika hilo kuendelea
kuwaelimisha wananchi juu ya athari na hatari ya kutumia mafundi wa mitaani
katika kuungiwa huduma hiyo jambo ambalo mara nyingi huleta hasara kutokana na
hitilafu zinazojitokeza baadaye.
No comments:
Post a Comment